Posts

Showing posts from March, 2025

"Safari ya Maarifa: Kuelimisha na Kusaidia Vijana Kupitia Blog Hii"

Rafiki yangu, nafurahi sana kukukaribisha kwenye blog hii! Leo ni siku ya kwanza kushirikiana nawe maarifa na uzoefu wangu, na ningependa kutumia fursa hii kueleza sababu kubwa iliyonisukuma kuanzisha safari hii ya kushirikisha elimu na maarifa. Kwa zaidi ya miaka tisa (9), nimekuwa nikifanya kazi kwa ukaribu na watoto na vijana balehe. Katika safari hii, nimejifunza mambo mengi kupitia vijana na watoto niliowasaidia kusonga mbele katika maisha yao. Nilipata msukumo wa kuwasaidia vijana wenzangu baada ya mimi mwenyewe kukumbana na changamoto za balehe, lakini kwa msaada wa wataalamu wa vijana, nilipata mbinu sahihi za kukabiliana nazo. Lengo langu ni kutumia ujuzi na uzoefu wangu kuleta mabadiliko chanya katika maisha ya watoto na vijana balehe kwa kusaidia ukuaji na ustawi wao. Kupitia blog hii, nitashirikisha makala mbalimbali kuhusu makuzi na malezi ya watoto na vijana balehe ili kuwasaidia kupita kipindi hiki cha mpito kwa usalama. Pia, tutapata nafasi ya kushirikishana uzoef...