Namna Gani Kijana Anaweza Kukabiliana na Msukumo Rika ili Kuvuka Kipindi cha Balehe Salama
Rafiki,
Kipindi cha balehe ni wakati wa mabadiliko mengi ya kimwili, kihisia, na
kiakili.
Katika
kipindi hiki, vijana hukutana na changamoto nyingi, na moja ya changamoto kubwa
ni msukumo wa rika. Huu ni ule ushawishi wa kutaka kufanya mambo fulani
kwa sababu marafiki au watu wa rika lako wanayafanya, hata kama ndani yako
unajua si sahihi.
Lakini swali ni hili: Unawezaje kukabiliana na msukumo huu na bado kubaki salama kwenye safari yako ya ukuaji?
1.
Jitambue na Uthamini Nafsi Yako
Kujitambua
ni msingi wa kila kitu. Jua wewe ni nani, unataka nini maishani, na uamue kuwa
hutafanya jambo lolote kwa sababu ya kushawishiwa tu.
Weka
misingi na maadili yako imara. Kumbuka, kuwa tofauti siyo dhambi, bali
ni ujasiri.
2.
Jifunze Kusema “Hapana” kwa Kujiamini
Kukataa
msukumo mbaya si udhaifu ni ujasiri. Jifunze kusema “Hapana, sihitaji kutumia
dawa za kulevya,” au “Hapana, sitashiriki katika tabia hatarishi.” Usiogope
kupoteza marafiki, marafiki wa kweli watakuheshimu kwa msimamo wako.
3.
Chagua Marafiki sahihi
Marafiki
zako wana nafasi kubwa katika maisha yako. Chagua wale wenye maono kama yako,
wanaohamasisha ndoto zako, si wanaokupeleka kinyume na dira yako. Kumbuka
methali isemayo, "ambaye hutembea na wenye hekima atakuwa na hekima,
bali rafiki wa wapumbavu ataumia."
4.
Zungumza na Wazazi/Walezi au Watu Wazima Unaowaamini
Kuna
nguvu kubwa katika kuzungumza. Ukijikuta kwenye hali ngumu ya kushawishiwa
vibaya, wasiliana na mzazi, mlezi, au mtu mzima unayemwamini. Watakusaidia
kukupa ushauri sahihi na kukuimarisha kiakili.
5.
Jihusishe na Shughuli Chanya
Jihusishe
na michezo, vikundi vya vijana, usomaji wa vitabu, muziki, sanaa, au kazi za
kujitolea. Shughuli hizi si tu zinakupa furaha, bali pia hukupa marafiki wenye
malengo kama yako, na kupunguza nafasi ya kushawishiwa vibaya.
6.
Tambua Athari za Msukumo Mbaya
Jua
kuwa baadhi ya matendo yanayoletwa na msukumo wa rika yanaweza kuharibu maisha
yako kabisa. Mimba za utotoni, magonjwa ya zinaa, utegemezi wa madawa ya
kulevya, kushindwa shule au hata kuingia kwenye uhalifu vyote vinaweza kuwa
matokeo ya kushindwa kupinga msukumo huu.
Balehe
siyo kipindi cha kubahatisha ni daraja la kuelekea utu uzima. Ili uvuke salama,
unahitaji msimamo, maarifa, na maamuzi sahihi. Msukumo rika unaweza kuwa
hatari, lakini ukiwa na dira, unaweza kuushinda na kusimama imara.
Kumbuka
kijana: “Wewe
ni kiongozi wa maisha yako. Usiache mtu mwingine ashike usukani wa ndoto zako.”
Comments
Post a Comment